Aliyekua kiungo wa klabu ya Arsenal, Ray Parlour anaamini mbadala wa meneja wa sasa wa klabu hiyo Arsene Wenger, anapaswa kuwa na mtazamo tofauti ili kuweza kufikia lengo la kurejesha taji la ligi ya nchini England klabuni hapo.

Parlour, amelizungumza jambo hilo, alipokua akijibu maswali aliyokua akiulizwa na mwandishi wa habari wa mtandao wa 365, juu ya mtazamo wa kikosi cha Arsenal kwa sasa, ambacho kimeonyesha kushindwa kufikia lengo la kutwaa ubingwa wa England.

Parlour, amesema ikitokea Arsene Wenger anaondoka klabuni hapo, viongozi wanapaswa kuwa na msimamo utakaoweza kuiweka Arsenal katika hali ya kiushindani zaidi, kwa kumpata meneja ambaye atawezana na mshike mshike wa ligi ya nchini England.

Hata hivyo alipoulizwa ni nani kwa upande wake anaamini anafaa kumrithi Arsene Wenger, mkongwe huyo ambaye alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa ubingwa wa England kwa mara ya mwisho huko jijini London, alisema Diego Simeone ana sifa zote za kuirithi nafasi ya babu huyo kutoka nchini Ufaransa.

Amesema Simeone amekua ni mtu wa tofauti katika soka la barani Ulaya kwa sasa, na anajua anachokifanya pale linapokuaja suala la ushindani, huku akitolea mfano kinachoendelea kwa sasa kwenye ligi ya nchini Hispania ambapo kikosi cha Atletico Madrid kinachonolewa na meneja huyo kutoka nchini Argentina kipo katika mbio za ubingwa.

Ray Parlour wakati akiitumikia Arsenal chini ya Arsene Wenger 

“Kwa hakika hakuna mwingine ninaemuona ambaye ataweza kuifikisha Arsenal inapotaka kufikishwa zaidi ya Simeone” Alisema Parlour

“Simeone amekua na sifa zote za kuongoza kikosi kama meneja na anajua namna ya kuhamasisha, jambo ambalo naamini akijanalo hapa Arsenal hakuna kitakachoshindikana katika kutatua kiu ya kutwaa ubingwa wa nchini England” Aliongeza Parlour

Parlour amezungumza mtazamo huo, huku kukiwa na shinikizo kubwa kwa meneja wa Arsenal, Arsenel Wenger kutoka kwa mashabiki na wanachama la kumtaka aondoke kwa kutumia kaulimbiu “Wakati Wa Mabadiliko”.

Wenger kwa mara ya mwisho alifanikiwa kutwaa taji la nchini England msimu wa 2003-04 akiwa na kikosi ambacho Parlour alikua mmoja wa wachezaji waliofanikisha mafanikio hayo ambayo yalipatikana kwa Arsenal bila kufungwa mchezo wowote wa ligi kwa msimu mzima.

Justin Bieber ajibu tuhuma za kujifananisha na Mungu
NATAKA KUWA KAMA TV YA NYUMBANI KWETU