Uwezo wa Raymond aka Rayvanny wa WCB umeendelea kuwa gumzo kwenye vinywa vya wajuzi wa masuala ya muziki, ambapo sasa hali hiyo imemfika mtayarishaji wa muziki wa Wasafi Records, Laiza.

Laiza amemtaja Rayvanny kuwa ndiye msanii ambaye anajisikia shangwe na ku-enjoy zaidi kufanya naye kazi za muziki kuliko wasanii wote wa kundi hilo lililo chini ya Bosi, Diamond aka Chibu Dangote.

“Nikiwa nafanya kazi na Raymond naenjoy zaidi,” Laiza alifunguka kupitia Twenzetu ya 100.5 Times Fm.

VIDEO: Azma afunguka alivyowachanganya ‘Sugu’ na Izzo B Kwenye Garagasha

Mtayarishaji huyo wa hits za wasanii wa WCB alisema kuwa Raymond pia ndiye msanii aliyeanza kuona uwezo wake na kumuamini kuwa anaweza kufanya kazi nzuri akiwa chini ya lebo hiyo kubwa zaidi nchini.

“Ni mtu ambaye alianza kuniona zaidi ya wasanii wote walioko pale, ukiacha Diamond,” alisema. “Naweza kusema ni mtu ambaye alisema kwamba ‘nina imani na huyu zaidi’. Na wimbo wake naweza kusema ndio uliofungua milango watu kunisikia zaidi,” aliongeza.

Hivi karibuni, mshindani mkuu wa Diamond, Ali Kiba alionesha wazi jinsi anavyoukubali uwezo wa Raymond kwa kuposti kwenye Instagram video inayomuonesha akiimba wimbo wa msanii huyo.

Hongera Leodegar Tenga - Rais Wa Heshima TFF
TFF Yavitahadhalisha Vyombo Vya Habari Kuacha Kampeni Chafu