Msanii kutoka WCB Wasafi ambaye pia ni boss wa Next Level Music Rayvanny ameonyesha kuchukizwa na mwenendo wa utamaduni mbaya wenye kusababisha kuwepo kwa chuki baina ya wasanii kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva ambao unachangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa makuzi ya tasni hiyo.

Rayvanny amekiri kuwa muziki wa kizazi kipya unaendelea kukua na kwamba anaimani kubwa muziki huo utafika mbali kwa wasanii kudumisha umoja na mshikamano utaopelekea kuondoa chuki iliyopo baina yao kama ilivyo kwa wasanii wa mataifa mengine.

“Muziki wetu unapoenda sio pabaya na utafika mbali tukiacha chuki na kuumia unapoona mwenzako anafanya vizuri, Wenzetu mmoja wao akifanya vizuri wote wanamsapoti basi nasisi tufanye kama wenzetu ili tufike mbali, NASAPOTI KILA ANAEFANYA VIZURI SABABU MMOJA AKIFANIKIWA IMEFANIKIWA INDUSTRY YETU LETS GO GLOBAL”

Ameandika rayvanny Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Donny asaka njia ya kuondoka Old Trafford
Meek Mill ahofia kutapeliwa