Msanii wa Bongofleva, Rayvanny ambaye usiku wa kuamkia leo Jini 25, 2017 ametwaa tuzo ya BET, kipengele cha ‘Viewers Choice Best New International Act’ pia akiwa msanii wa kwanza kutoka Bongo kutwaa tuzo hiyo ametoa maneno mazito ya shukrani kwa msanii Hamad Ally maarufu kama Madee akikumbuka jinsi alivyokuwa msaada kwake.

Wengi baada ya mafanikio ni vigumu sana kukumbuka maisha ya nyuma na kuwashukuru waliowasaidia, lakini imeonekana tofauti kwa Rayvanny ambaye ameandika maneno yaliyoonekana kujawa na hisia kubwa kupitia ukurasa wake wa Instagram, amekumbuka kipindi cha miaka sita iliyopita jinsi Madee alivyokuwa sehemu ya mafanikio yake baada kumsaidia katika maisha ya kawaida hata kimuziki pia kipindi anaanza kufika Dar es salaam.

Amesema miaka sita iliyopita ikilikua kipindi kigumu sana kwake sababu alikua mgeni Dar as salam, alikosa hata nguo za kuvaa lakini Madee alisimama naye na kila wakati walikuwa wote baada ya kumuona mnyonge asie na msaada.

“Kuna kipindi nilikosa hata nguo zakuvaa, alikua akinipa hata nguo alizokua akizipenda yote kunistiri mdogo wake”

“Nakumbuka Miaka Sita Iliyopita ndio kipindi Ambacho nilikutana na Madee. Kipindi hicho Sikujua nilichonacho pia sikujua Wapi nianzie na nini nifanye. Kilikua kipindi kigumu sana Kwangu sababu nilikua Mgeni Dar as salam. Lakini kaka angu @madee alisimama namimi Kila Alipokua Akienda Alienda na mimi na hii yote ni baada yakuniona mnyonge Nisie na msaada.”

“Nilijuana na Wadau na baadhi ya wasanii Kupitia kaka angu @madeeali Pia Alikua akinipeleka studio nakunishauri Vitu vingi sana vyakimaisha na mziki pia Nimepata Uzoefu Mkubwa wakutumbuiza mbele ya kundi lao watu kutoka kwake. Kuna kipindi nilikosa hata Nguo zakuvaa Alikua akinipa hata nguo alizokua akizipenda yote kunistiri mdogo wake.Nakumbuka kuna kipindi Akasema mdogo wangu Ray jifunze gari, nikamkatalia nakumwambia kwamba mimi ntaendesha Wapi gari na Ntakuja lini kupata gari ila Ananiambia mdogo wangu Unakitu Ambacho kitakusaidia baadae yote yatawezekana.”

“Alianza kunifundisha Gari yake japo nilikua naigongesha gongesha kwenye mashimo sababu nilikua sijui lakini Alinivumilia hadi nikajua Pia Nikawa mjanja wavitu vingi na kujiamini kisa yeye. Siku Nilipomwambia Naenda Wasafi nilijua hatonielewa Lakini Ndio Alikua mstari Wa mbele mambo yangu yafanikiwe nae Akichangia mpaka #Raymondtiptop Akawa #Rayvanny Hadi leo Hii Tumechukua Tuzo kubwa duniani #BETAwards MUNGU AKUBARIKI KWA MOYO HUO HUO SINA CHA KUKULIPA MUNGU PEKEE NAKUSHUKURU WEWE NA FAMILIA NZIMA YA SENEDA…. HUU MWANZO MUNGU MWEMA @madeeali” ameandika Rayvanny

 

Nakumbuka Miaka Sita Iliyopita ndio kipindi Ambacho nilikutana na Unaemuona mbele yangu.kipindi hicho Sikujua nilichonacho pia sikujua Wapi nianzie na nini nifanye.Kilikua kipindi kigumu sana Kwangu sababu nilikua Mgeni Dar as salam.Lakini kaka angu @madeeali Alisimama namimi Kila Alipokua Akienda Alienda na mimi na hii yote ni baada yakuniona mnyonge Nisie na msaada.Nilijuana na Wadau na baadhi ya wasanii Kupitia kaka angu @madeeali Pia Alikua akinipeleka studio nakunishauri Vitu vingi sana vyakimaisha na mziki pia Nimepata Uzoefu Mkubwa wakutumbuiza mbele ya kundi lao watu kutoka kwake.Kuna kipindi nilikosa hata Nguo zakuvaa Alikua akinipa hata nguo alizokua akizipenda yote kunistiri mdogo wake.Nakumbuka kuna kipindi Akasema mdogo wangu Ray jifunze gari,nikamkatalia nakumwambia kwamba mimi ntaendesha Wapi gari na Ntakuja lini kupata gari ila Ananiambia mdogo wangu Unakitu Ambacho kitakusaidia baadae yote yatawezekana.Alianza kunifundisha Gari yake japo nilikua naigongesha gongesha kwenye mashimo sababu nilikua sijui lakini Alinivumilia hadi nikajua Pia Nikawa mjanja wavitu vingi na kujiamini kisa yeye.Siku Nilipomwambia Naenda Wasafi nilijua hatonielewa Lakini Ndio Alikua mstari Wa mbele mambo yangu yafanikiwe nae Akichangia mpaka #Raymondtiptop Akawa #Rayvanny Hadi leo Hii Tumechukua Tuzo kubwa duniani #BETAwards MUNGU AKUBARIKI KWA MOYO HUO HUO SINA CHA KUKULIPA MUNGU PEKEE NAKUSHUKURU WEWE NA FAMILIA NZIMA YA SENEDA…. HUU MWANZO MUNGU MWEMA @madeeali

A post shared by Raymond (@rayvanny) on

Jeshi la Polisi latoa tahadhari kwa watumiaji wa barabara
Lowassa aimulika ‘kamatakamata’ viongozi wa Chadema, asema imetosha