Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amebainisha mtandao wa watu waliokutana na dereva ‘taxi’ aliyembeba mgonjwa wa corona aliyepatikana Jijini Arusha baada ya kumpata dereva huyo.

Gambo amesema kabla ya dereva huyo kurudi nyumbani kwake, aliwabeba abiria wawili na kuwapeleka Karatu kwenye kituo cha watoto cha ‘mwema children center ‘ambao tayari timu ya madaktari imetumwa kuchukua vipimo vyao na kuwataka wasitoke nje ndani ya siku 14.

Amesema baada ya kumpata dereva wamechukua ‘sample’ ya vipimo ambayo tayari imepelekwa kwenye maabala kuu, lakini wameanza kufuatilia mtandao wa pili ambao ni familia yake na watoto ambao asubuhi walienda shuleini.

” Mara baada ya kumshusha mama Isabella aliweza kwenda nyumbani kwake ambapo ana mke wake na anawatoto wa nne na wote alishikana nao kama sehemu ya familia. watoto walivyo amka asubuhi walienda shuleni”. Amesema RC Gambo.

Aidha ametoa msisitizo kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kuto taharuki, kwani sababu za kisayansi bado hazijathibitisha kama ugonjwa huu unaambukizwa kwa njia ya hewa na kuwataka wananchi kuendelea kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.

Tahadhari ya Corona, CCM yasitisha mikutano ya ndani na hadhara
Kesi ya Zitto Kabwe kuanza kuunguruma kisutu leo