Mkuu wa Mkoa Kagera Brig.Jen. Marco Gaguti amemuagiza kamanda wa polisi mkoani humo pamoja na Kamanda wa TAKUKURU kuwakamata watumishi 34 katika halmashauri ya wilaya Biharamulo wakiwemo watendaji wa vijiji na kata kwa kushindwa kurejesha fedha shiligi milioni 307 zilizokusanywa kutoka vyanzo vya mapato ya ndani bila kupelekwa Benki.

Agizo hilo amelitoa leo, juni 23 mwaka huu alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo iliyolenga kutoa maelekezo ya kiutendeji kutokana na halmashauri hiyo kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato na kuoneka kuna ubadhilifu wa fedha za serikali.

Mku huyo pia licha ya kuagiza kukamatwa na kuwekwa chini ya ulizi watumishi hao, ameziagiza mamlaka kuwasimamisha kazi kaimu muwekahazina Sospiter Makene, Jastine Banula afisa Tehama, Rogers Semukoko afisa tehama na Beatrice Gurusya afisa biashara wote wakiwa ni watumishi wa halmashauri hiyo.

Gaguti amechukua uamuzi huo baada ya kutoa siku saba kwa watumishi hao kurejesha fedha hizo kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika juni 05 mwaka huu kilichokuwa kina lengo la kujibu hoja za mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali.

“Nilikuja hapa nikatoa maelekezo kwa wale wote waliokuwa wanakusanya fedha kwa kutumia mashine za Poss bila kuzipeleka benki kuwa warejeshe fedha na nikawapa siku 7 lakini fedha iliyorejeshwa ni asilimia 2%, kwa mwendo huu hatuwezi kwenda lazima tuweke misingi imara ya kuboresha utumishi na uadilifu” Amesema Gaguti

“hapa nina orodha ya watendaji 30 ambao nampatia kamanda wa polisi kuhakikisha watu hao wanakamatwa popote walipo na wengine wanne hawa naagiza wasimamishwe kazi lakini wawe chini ya uangalizi wa kamati ya ulizi na usalama ili kutoa ushirikiano.” Amefafanua Mkuu wa mkoa Gaguti.

Ameongeza kuwa watumishi wa umma wanatakiwa kuwa waadilifu na kuiogopa fedha ya serikali na kuahidi kuwachukulia hatua wote watakao bainika wakifanya vitendo vya ubadhilifu na kutoa onyo kali kwa watendaji wa vijiji na kata mkoani humo kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali.

“Fedha ya serikali ni ya moto hivyo haipaswi kula niwasihi tu ndugu zangu tusijaribiane, hatutasita kumchukulia hatua yeyote atakayehusika na upotevu wa pesa, tambueni watendaji ndiyo mnadhamana ya kukusanya mapato ya ndani kutoka katika vyanzo vya mapato katika maeneo yenu.” Ameeleza Gaguti.

Aidha Gaguti amesema kuwa kuna baadhi ya watumishi walikataa kusajili vyanzo vya mapato kwa makusudi na baadae kuwarudia wafanyabiashara na kuchukua fedha kinyemela na kusababisha serikali kukosa mapato yake.

Gazeti la Tanzania Daima lafungiwa
Kurzawa kuzigonganisha Arsenal, Chelsea