Mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila amedhamiria kuwatumia wasomi na wataalamu wa mkoa huo kuhakikisha anauendeleza kiuchumi na kidiplomasia.

Chalamila ametoa kauli hiyo Agosti 04, mara baada ya kukabidhiwa ofisi na mtangulizi wake Meja Jenerali Charles Mbuge katika hafla iliyofanyika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Kagera.

Amesema ili kuifikia adhma ya Rais Samia ya kuhakikisha mkoa huo unakua kiuchumi atahakikisha anawatumia wasomi ambao ni wazawa wa Kagera ambao wataweza kumpatia mawazo ya namna bora ya kufanikisha hilo.

“Mkoa huu unao wasomi wengi, wapo maprofesa, madaktari na watafiti wengi, nitawatumia wataalamu hao kupitia tafiti zao kuhakikisha mkoa huu tunauendeleza kiuchumi ili kufikia adhima ya Mhe. Rais Samia ya kuufungua mkoa huu kiuchumi,” amesema Chalamila.

Kuhusu mipaka ya mkoa huo Chalamila amesema kuwa atahakikisha ulinzi unaimarishwa hususani kwa nchi zinazopakana na Tanzania kwa upande wa Kagera.

Kwa upande wake aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge amemsihi mkuu mpya wa mkoa kuhakikisha anasimamia miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na kukamilika kwa wakati na kuendana na thamani ya fedha iliyotolewa huku akimkumbusha kusimamia zao muhimu la Kahawa.

Wajawazito Meta kujifungua pamoja na wenza wao
Simba SC yafunguka sakata la JEZI mpya