Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amewataka wajumbe wa Bodi ya Barabara kuhakikisha vipaumbele vya Ujenzi wa Barabara vinazingatia mahitaji ya wananchi.

Kunenge amesema hayo wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es salaam ambapo amesema kumekuwa na ujenzi wa Barabara ambazo sio kipaumbele cha wananchi na kuacha zile zenye uhitaji zikibaki kuwa mbovu, jambo linalosababisha kero kwa watumiaji.

Aidha, Kunenge amesema kuanzia sasa ikitokea vikao vimepitisha mambo yasiyozingatia mahitaji ya wananchi walio wengi, yatakapofika mezani kwake hatoyaidhinisha kwa kuwa ameamua kuwa sauti ya walio wengi.

Katika hatua nyingine Kunenge ameonyesha kuchukizwa na tabia ya baadhi ya viongozi wanaochelewa kuhudhuria kwenye vikao na kusababisha vikao kuchelewa kuanza kitendo alichokiita utovu wa nidhamu.

World Vision yaadhimisha miaka 40 kwa kutoa madawati 350
Wanafunzi 1,194 wakatisha masomo kwa ujauzito