Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameshangazwa na kitendo cha Kenya kuzuia bidhaa aina ya unga wa ngano,  kutoka Tanzania kuingizwa nchini humo kwaajili ya kuuzwa.

Ameyasema hayo mara baada ya kutembelea mpaka wa Namanga na kusikitishwa na kitendo cha malori zaidi ya 40 yaliyobeba unga wa ngano ya wafanyabiashara toka Tanzania yaliyokua yakielekea nchini Kenya kuzuiliwa kuingia nchini humo.

Gambo ameshangazwa na kitendo cha nchi ya Kenya kuendelea kuzuia bidhaa toka Tanzania ilhali bidhaa toka Kenya huruhusiwa kupita katika mpaka huo hali ambayo amesema imewasababishia hasara kubwa wafanyabiashara wa Tanzania.

“Hapo katikati kumekua na changamoto lakini pande mbili zilishakaa na kwa upande wa Tanzania vizuizi vyote vilishaondolewa, bidhaa zinazotoka Kenya kuja kwetu zinapita vizuri, sasa nashangaa kwanini wao bado wanazuia bidhaa zetu,”amesema Gambo

Naye Kaimu Afisa forodha wa mpaka huo upande wa Tanzania, Mohamed Tukwa amesema kuwa licha ya kufanya jitihada mbalimbali za kuwasiliana na wenzao wa upande wa Kenya bado hakuna suluhu ya kuruhusu bidhaa hizo kuingia nchini Kenya.

Hata hivyo,  baadhi ya madereva wa malori wanaolekea nchini Kenya wamedai kuwa hadi sasa hawajui kinachoendelea kwani wapo hapo kwa takribani siku nane hali ambayo wanadai imewasababishia usumbufu mkubwa.

Video: Naj wa Baraka the Prince atimba na 'Utanielewa'
Sethi anyimwa kutibiwa nje ya nchi