Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo amewataka wadau wa elimu kuunganisha nguvu zao katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo ili kufikia malengo ya Serikali ya ufaulu wa asilimia 80 kila wilaya.

Ameyasema hayo wakati wa kikao chake na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri ,Maafisa Elimu wa Shule za Sekondari na Msingi pamoja na wadau wengine wa Elimu.

Gambo amesema ili kufikia malengo ya Matokeo Makubwa sasa(BRN) yanayotaka ufaulu katika ngazi ya elimu ya msingi na Sekondari kufikia asilimia 80 lazima kuwepo na vifaa vinavyohusika kwa ajili ya  kufundishia na kujifunzia.

“Katika kuangalia elimu kwa mapana yake, hatuna budi kuwajengea uwezo walimu wetu kwa kuwapa mafunzo ya mara kwa mara ili kuwapa motisha badala ya kuwaacha na elimu waliyoipata Chuoni pekee,” amesema Gambo

 

Ally Star: Taarabu itakufa tusipoisaidia
Majaliwa akagua Maghala ya mahindi jijini Dar