Mkuu wa mkoa wa Mara Ally Hapi amewataka wananchi kupuuza taarifa za upotoshaji zinazosambazwa na baadhi ya watu kuwa serikali imerejesha Ada Mashuleni na kuonya kuwa watu hao wanapaswa kuchukuliwa hatua kali kwa kusambaza uzushi huo.

RC Hapi ametoa kauli hiyo wakati akikabidhiwa madarasa 113 yanayotokana na fedha za maendeleo na Uviko-19 ambapo wilaya ya Rorya ilipokea kiasi cha shilingi Bilioni 2.3.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Salum Hapi amekabidhiwa vyumba vya Madarasa 113, Sekondary 98 na Shikizi 15 vilivyoambatana na ofisi 44 ambazo Wilaya imejenga

Katika ziara yake hiyo Hapi amewataka wazazi kuandikisha watoto kuandikisha watoto wao shule na kupuuza taarifa zinazosambazwa mtaani kuwa serikali imerejesha ada mashuleni.

Naye mMkuu wa Wilaya ya Rorya Juma chikoka amesema fedha hizo zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassani amesema wanafunzi Elfu saba 219 waliandikishwa katika wilaya ya Rorya watasoma bila kikwazo chochote.

Kanye West mikononi mwa polisi
Waziri Bashungwa atoa maagizo kwa maaafis wa elimu