Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa amewaahidi wakazi wa mkoa wa Kagera kusimamia vyema miradi na fedha zitakazotolewa kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha zinaleta maendeleo katika mkoa huo.

Mwasa ameyasema hayo hii leo Machi 24, 2023 mbele ya waandishi wa habari wakati alipowasili kwa mara ya kwanza katika ofisi yake ya mkoa, iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera.

Amesema “kubwa ninaloliomba kwa wanakagera wenzangu wote watumishi na wananchi ni ushirikiano, niwahaidi kwamba mimi pamoja na wenzangu tutafanya kazi njema na maendeleo Kagera yataonekana kwani Dkt Samia Suluhu Hassan ana mipango, ndoto na dhamira na Kagera kwahiyo hizo fedha nyingi anazowekeza tutajitahidi kuisimamia miradi itokee kwa viwango vilivyo bora kabisa”.

Fatma Mwassa, amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Mei 15 mwaka huu huku pia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Albert Chalamila kuhamishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Robertinho kutumia saa 216 Simba SC
Ulinzi waimarishwa Kambini Young Africans