Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanueli Maganga ameagiza kusitishwa mara moja shughuli za Kilimo katika msitu wa Kagerankanda wakati uongozi wa mkoa huo ukikamilisha mipango na taratibu za ugawaji wa maeneo ya msitu huo uliotolewa kwa wakulima na rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Amewaagiza viongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Wilayani Kasulu kuharakisha taratibu za kubaini na kupima sehemu ya eneo la msitu wa Kagerankanda ili wananchi waweze kugawiwa na kuanza shughuli zao za kilimo.

Maganga ametoa maelekezo hayo Wilayani kasulu ikiwa ni utekelezaji wa tamko la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa wakati wa ziara yake Mkoani Kigoma mwezi Juni mwaka huu.

“Hakuna mtu aliyemshawishi Rais kutoa eneo hilo kwa wananchi bali huo ni utashi wake na mapenzi yake kwa wananchi wa Kasulu hivyo waache kujitafutia umaarufu kwa kuwadanganya wananchi,” amesema Maganga.

Aidha, msitu wa Kagerankanda umekuwa ukiharibiwa kwa shughuli za kilimo kutokana na ardhi ya eneo hilo kuwa na rutuba na hali ya kustawisha mazao kwa wingi na kwa uhakika.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kuwa baada ya kamati kumaliza kazi za kupima na kubaini mahitaji ya ardhi kulingana na eneo litakalotolewa, taratibu za kugawa zitazingatia sheria ya ardhi namba 4 & 5 ya mwaka 1999.

Video: Usiyoyajua sakata la shamba la Sumaye, Uchunguzi 'Makinikia' almasi pasua kichwa
Makamanda Zimamoto wapanguliwa