Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amesikitishwa na tukio la mauaji ya Afisa Mtendaji wa Serikali ya mtaa wa Msumi mbezi yaliyofanyika siku ya Jumatatu na kuagiza wote waliohusika na mauaji hayo kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

RC Makalla ametoa maagizo hayo alipotembelea ofisi ya Mtaa huo na nyumbani kwa Marehemu kutoa mkono wa pole.

Makala ameagiza kila ofisi ya serikali ya mtaa na kata ilindwe na Askari mgambo nyakati za kazi ili kupunguza matukio ya hatari na ya kinyama ambayo viongozi wanakutana nayo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa amesema msako umefanikisha kuwakamata watuhumiwa wawili na upelelezi unaendelea ili kuchukua hatua.

Tukio hili la Mauaji ya Afisa Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Msumi linahusisha watuhumiwa watatu wanaosadikiwa kuwa na sababu za migogoro ya Ardhi.

Vijana watakiwa kuwa sehemu ya suluhu kwa matatizo ya waafrika.
Watanzania waishio nje ya nchi kupewa hadhi maalumu