Takwimu za wananchi waliopata chanjo ya UVIKO-19 zimeendelea kuongezeka kwa Kasi kufuatia jitihada za utolewaji wa elimu na ushawishi kwa jamii ambapo wananchi Milioni tatu na laki nne wamepata chanjo hiyo ikiwa ni ongezeko la wananchi kutoka milioni tatu na laki tatu kwa malengo yaliyowekwa mkoani Dar es Salaam.

Hayo ymesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla wakati wa matembezi ya hiari yenye lengo la kukuza uelewa na muitikio wa chanjo ya UVIKO-19 kwa Umma, yaliyoandaliwa na Hospitali ya Aga Khan Tanzanzia, Umoja wa Ulaya (EU), na Mashirika ya kimataifa ya maendeleo ya Aga Khan (AKDN).

RC Makalla amewataka wananchi wake kuendelea kupata chanjo ya UVIKO-19 ili kulinda afya zao na kuondokana na madhara mabaya yanayoweza kujitokeza kwa kutochanja ikiwa ni pamoja na kifo.

“Tuendelee kuhamasishana kupata chanjo ya UVIKO-19 na wengine waige mfano wa Agha Khan wa kuelimisha watu kujikinga na maradhi” amesema Rc Makalla.

“Ninashukuru European union kwa mchango mkubwa wa fedha, mmeshirikiana na serikali, wizara ya afya na mkoa wa Dar es Salaam kukarabati jengo la wazazi Amana, mmetoa mafunzo kwa watumishi wa Afya hivyo naamini kwa kushirikiana na nyinyi pamoja na aghakhan tutafanya mambo mengi sana” amesema Rc Makalla.

Katika hatua nyingine, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa ya kupata chanjo na kuleta Chanjo za kutosha ambazo zimesaidia nchi yetu kuto kutengwa na kuwa sehemu ya Dunia kwa kuwa ilikuwa vigumu mtu kusafiri bila kuchanjwa.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume amesema muitikio wa uchanjaji kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni mkubwa na kutaka kasi ya Uhamasishaji na uelimishaji wa jamii juu ya Umuhimu wa Chanjo ya Uviko-19 izidi kuendelezwa.

Dkt. Mfaume aliwashukuru Aga Khan kwa kufanya ukarabati katika hospitali ya Amana katika jengo la kuhudumia wagonjwa wa dharura wa mifumo ya upumuaji na kuweka vifaa vya kisasa, kuwajengea uwezo watumishi namna ya kutumia mashine hizo na namna ya kutoa huduma vizuri.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tiba, huduma za Aga Khan Tanzania, Dkt. Harrison Chuwa amesema, Mtandao wa Mashirika ya Kimataifa ya Aga Khan waliingia makubaliano ya mradi wa Pauni Milioni 9.4 unaolenga kuboresha miitikio ya kimfumo na ambayo inazingatia jinsia ili kushinda madhara ya kiafya, kiuchumi na kijamii yaliyosababishwa na gonjwa la UVIKO-19 katika nchi za Tanzania, Kenya , Uganda na Msumbiji.

Aidha amesema kuwa, huo ambao ulianza mwaka 2020 na kutarajiwa kumalizika mwaka 2023 ambapo kwa Tanzania unawekeza Bilioni 3.8 katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi na Mwanza

Mradi huo unatarajia kuhudumia watu zaidi 700,000 kwa kutekeleza mikakati ya kukabiliana na UVIKO-19 kwa wanaume na wanawake walio hatarini na kuunda mfumo wa utoaji huduma za afya kwa ajili ya usimamizi fanisi wa UVIKO-19.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 28, 2022
Nguema ashinda muhula wa sita nchini Guinea ya Ikweta