Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amepiga marufuku ufanyaji wa Biashara Kwenye maeneo hifadhi ya barabara zote za Mkoa huo baada ya utaratibu huo kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani na ongezeko la ajali.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipotembelea Soko la Kariakoo na kujionea Kero ya Ufanyaji biashara holela Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.

Kutokana na hilo RC Makalla amewaelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kufanya kikao na Wafanyabiashara hao Jumatatu ya September 13 na kuainisha maeneo ya kuwapeleka wote waliovamia hifadhi ya Barabara.

Aidha RC Makalla amewaelekeza Kuangalia utaratibu mzuri wa kufunga na kufungua baadhi ya Mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya biashara Kutokana na ufinyu wa maeneo ili Waweze kupata riziki.

Hata hivyo RC Makalla amesema kwa tathimini aliyofanya amebaini Hali ya Ufanyaji biashara holela Dar es salaam ipo kwa kiwango kikubwa na kuwanyima watembea miguu haki zao za msingi.

Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Manispaa zote za Mkoa huo kuweka Vibao vya kuzuia biashara Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.

Suluhu yapatikana kuwathibiti viboko ndani ya bwawa la Mtera
Africa-Shenzhen Economic & Trade Cooperation and Exchange Series Conference – Dar es Salaam,