Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa maagizo ya uvaaji barakoa katika vyombo vya usafiri wa daladala kwa kila mwananchi.

Akitoa maagizo hayo Rc Makalla amesema kuwa kuanzia sasa lazima kila mtu anayepanda kwenye chombo cha usafiri avae barakoa, na kwa vyombo vya usafiri (daladala) kupakia abiria kutokana na idadi ya viti.

Aizungumza na waandishi wa habari RC Makalla amesema kuwa maagizo hayo yana lengo la kuzuia maambukuzi ya virusi vya corona, nakusisitiza kuwa yoyote asiye na barakoa kutokupanda chombo cha usafiri.

 
Kwa upande wa taasisi pamoja na ofisi zilizopo mkoani Dar es Salaam, RC Makalla ameagiza kuwepo na sehemu za kutakasa mikono na watu wote wavae barakoa.

Hersi: Tuna kikosi kipana
Kiwango cha watumiaji wa bangi chaongezeka