Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amelielekeza Jeshi la Polisi kufanya msako wa kuwakamata Vibaka wanaofanya vitendo vya kihalifu ikiwemo kuiba na kupora Mali za Wananchi.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo baada ya kupokea malalamiko juu ya uwepo wa vijana wanaopora mali za wananchi na kuhatarisha usalama.

Kutokana na hilo RC Makalla pia amewataka wazazi kuchunguza mienendo ya vijana wao na kuwakanya mara moja ili wasiingie Katika mikono ya Sheria.

Hata hivyo RC Makalla ameelekeza kuanza kwa operesheni ya kukamata Vibaka na wahalifu Katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa hitimisho la ziara ya kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi Jimbo kwa Jimbo ambapo kesho atakuwa akisikiliza kero za Wananchi wa mabwepande.

DPP afuta kesi ya Lissu na wenzake
Young Africans yaweka rekodi 2020/21