Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amezindua kampeni ya usajili wa walipakodi wapya ikiwa ni utekelezaji wa wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutanua wigo wa ukusanyaji wa kodi.

Makalla ametoa wito kwa wafanyabiashara ambao bado hawajasajili biashara zao kuzisajili ili waweze kutambulika na kutimiza takwa la kisheria la ulipaji wa Kodi.

Aidha, amewataka wafanyabiashara kutunza kumbukumbu ili kurahisisha zoezi la ukadiriaji na ukusanyaji wa kodi na kuwasisitiza kutoa risiti wanapouza na wananchi kudai risiti.

Pamoja na hayo RC Makalla ameipongeza TRA kwa mapinduzi makubwa katika ukusanyaji wa kodi, jambo lililowezesha mapato kupanda na kuwezesha Serikali kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo.

Hata hivyo ameonyesha kuchukizwa na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wanaowatumia wamachinga kukwepa kodi na kuikosesha Serikali mapato.

Zoezi la usajili walipakodi wapya limezinduliwa Mkoa wa Dar es Salaam na litatekelezwa nchi nzima ambapo TRA itakuwa ikitoa namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) bure pamoja na Tax Clearence kwa wafanyabiashara wapya lengo likiwa ni kuongeza mapato.

Makambo atimba kambini Avic Town
Wazee wapewa kipaombele chanjo ya Uviko 19