Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imeandaa mkakati endelevu wa kuifanya Dar es Salaam kuwa safi kwa kuwa na kampeni ya kufanya usafi yenye kauli mbiu ya Safisha pendezesha Dar es Salaam.

Aidha RC Makalla amewaalika wananchi wote kushiriki kwenye kampeni hiyo ambapo kampeni hiyo itazinduliwa Novemba 22, 2021 na kuanza kufanya kampeni ya usafi kwa pamoja kuanzia Novemba 4, 2021 wiki ya kuelekea Uhuru wa Tanzania.

Ameongeza kuwa muendelezo wa kampeni ya kuiweka Dar safi ni zoezi endelevu, ambapo Kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kuanzia saa 12 asubuhi mpka saa tatu asubuhi itakuwa ni nafasi ya Kila jamii kushiriki usafi kwa maeneo yanayowazunguka.

Baada ya kuwa katika mazingira ya ufanyaji biashara holela mazingira yetu kumekuwa na uchaguzi mkubwa wa mazingira mitaro yetu mingi iliziba kwaiyo baada ya zoezi la upangaji vizuri wafanyabiashara wadogo tumepata nafasi ya kufanya usafi Mkoa wa Dar es Salaam,” Amesema RC Makalla.

Sambamba na hayo yote amewahasa wananchi wa Dar es Salaam kushiriki kikamaligu katika kampeni hiyo yenye kauli mbiu ya Safisha pendezesha Dar es Salaam.

Wizara ya Afya yapokea dozi zilizotelekezwa bandarini
Kamala Haris akabidhiwa mamlaka ya Rais Marekani.