Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amefanya Mazungumzo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki kuhusu Hali ya Ubovu na uchakavu wa Mnada wa Pugu na jitiada za kuboresha Machinjio hiyo kuwa ya kisasa kuendana na hadhi ya Jiji la Dar es salaam.

Mazungumzo hayo yamekuwa na mafanikio makubwa baada ya Waziri Ndaki kumkabidhi RC Makalla jukumu la kumsimamia na kumbana Mkandarasi amalize kazi ya kuboresha Mnada huo Kufuatia Mkuu wa Mkoa kutoridhishwa na Hali ya Mnada huo wakati alipofanya ziara mnadani humo hivi karibuni na kujionea Kero lukuki.

Kutokana na hilo Sasa RC Makalla ameahidi kumsimamia ipasavyo mkandarasi kukamilisha maboresho ya Mnada kwa wakati ili kupunguza changamoto zilizokuwa zikiwakabili wafugaji na Wafanyabiashara Katika Mnada huo.

Aidha RC Makalla amesema Kama Mnada huo utakuwa Katika Hali nzuri itasaidia pia Machinjio ya kisasa Vingunguti kupokea mifugo yenye ubora na kusaidia upatikanaji wa Nyama Bora.

Hayo yote yamejiri wakati wa mkutano wa Wadau wa sekta ya Mifugo uliofanyika leo Jijini Dar es salaam ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

Uongozi wa kijeshi Guinea kuunda Serikali ya mpito
Ratiba ya FIFA yaivurugia Azam FC