Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amezindua rasmi Safari ya Kupendezesha Mandahari ya Jiji Hilo kwa Kupaka rangi za Bendera ya Taifa kwenye Vyuma na Minyororo kwenye Barabara kuu pamoja na kupanda Miti na maua kwenye bustani.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Kupendezesha lililoanzia Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere RC Makalla ametoa onyo Kali kwa watu watakaoharibu au kuiba Vyuma hivyo.

Aidha RC Makalla amezielekeza Halmashauri zote kusimamia Vyuma vilivyowekwa na kutunza bustani zisiharibiwe huku akitoa wito kwa Wananchi kufanya Usafi wa mazingira.

Kuhusu mahadhimisho ya Miaka 60 Uhuru yanayotaraji kufanyika Disemba 09, RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye Sherehe hizo zitakazofanyika Uwanja wa Uhuru zikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na hayo RC Makalla ameendelea kuwasisitiza Wakandarasi wa Usafi kuhakikisha wanazoa taka zilizokusanywa na Wananchi kwa wakati.

Singo: Maandalizi Mchezo wa Miaka 60 ya Uhuru, Tanzania Vs Uganda
Shaffih Dauda aukomalia udhamini wa GSM