Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru zinazotaraji kufanyika Disemba 09 kwenye Uwanja wa Uhuru.

RC Makalla ametoa wito huo wakati wa kikao Cha pamoja na Watendaji wa Kata na Mitaa kilichoketi leo kuweka mikakati ya Maandalizi ya Sherehe hizo ambazo zitakuwa za kwanza kwa Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha katikati kuelekea Sherehe hizo zitatanguliwa na uzinduzi wa Miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa wa Da es Salaam.

Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru zitahudhuriwa na Wakuu wa Nchi mbalimbali watakaowasili nchini kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na Wananchi wa Tanzania.

Kauli Mbiu ya siku ya Uhuru wa Tanzania mwaka huu ni “Miaka 60 ya uhuru: Tanzania Imara, Kazi Iendelee.”

Marufuku kutoa taarifa za harakati za kijeshi Ethiopia
B.1.1.529: Aina mpya ya Kirusi cha Corona inayoathiri vijana zaidi