Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametoa mwezi mmoja kwa Manispaa ya Kinondoni kuanza ujenzi wa mradi wa ufukwe wa Coco Beach, kwa kile alichokidai kuwa Manispaa hiyo imekuwa ikichelewesha mradi huo.

Ametoa agizo hilo jijini Dar es salaam, wakati alipotembelea eneo la ufukwe wa Coco Beach, ambapo amesema kuwa Manispaa hiyo imekabidhiwa Bilioni 14, lakini mpaka sasa wanaishia kufanya vikao tu.

Amesema kuwa eneo hilo la Coco Beach limerudishwa kuwa eneo la umma, ili watu waende kupumzika, na Rais Magufuli tayari alishatoa bilioni 14, ili kuanza kuijenga Coco, lakini kwa masikitiko makubwa mpaka sasa ujenzi haujaanza.

“Moja ya mambo yaliyonishangaza ni mshauri waliyempata ameacha mchoro wa bilioni 14, amekuja na mchoro wa bilioni 40, tumewapa muda wa mwezi mmoja ili Coco Beach ianze kujengwa, haiwezekani fedha imetolewa miradi haiendi, hatuwezi kukubali Rais wetu aendelee kuhujumiwa, natoa mwezi mmoja muanze kushughulikia ujenzi” amesema Makonda.

Katika ziara hiyo Makonda amewataka viongozi wa Manispaa ya Kinondoni kuendana na kasi ya ujenzi wa daraja la Selander, ambapo amependekeza mpaka mradi wa daraja hilo kukamilika na uboreshaji wa ufukwe wa Coco Beach uwe umekamilika

Mfumuko wa bei kwa mwezi julai 2019 wabaki asilimia 3.7
Video: Willy Paul, Ali Kiba na Ommy Dimpoz waachia ‘Nishikilie’, iangalie hapa