Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam na kusababisha vifo vya watu saba, Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda ameagiza wanafunzi wasiende shule kwa siku mbili kupisha mvua hizo zilizosababisha mafuriko.

Hata hivyo Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,  TMA, imesema mvua kubwa zitaendelea kunyesha mpaka mwezi Mei, mwaka huu, hivyo imewataka watu kuchukua tahadhari mapema.

Pia TMA imeeleza kuwepo kwa vipindi vifupi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Morogoro, Dar es salaam, Pwani, Tanga, Lindi, Mtwara, Pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Kigoma, Tabora, Katavi, Kilimanjaro, Arusha, na Manyara.

”Kwa Tarehe 16/04/2018 Kuna muendelezo wa tahadhari na Agalizo la Matarajio ya kuwepo kwa vipindi vifupi vya mvua kubwa”.

Imeandika TMA katika tovuti yake.

Aidha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam yameathirika na mvua zinazoendelea kunyesha mfululizo, Jeshi la Polisi limetaja maeneo ya Magomeni na Jangwani na kuripoti kuwa baadhi ya wakazi wamekimbia makazi yao.

 

 

Msigwa akanusha JPM kupokea tuzo ya kiongozi bora barani Afrika
Aliyedai kutelekezwa na Lowassa aomba radhi

Comments

comments