Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amewaweka ndani Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Boniphace Magesa na Ofisa Ardhi wa Halmashauri hiyo Peter Mkalipa kwamadai ya kuvidanganya vyombo vya Serikali.

Mongela aliamua kuwaweka ndani watendaji baada ya Waziri Jafo kutoridhishwa na majibu kuhusu madai ya Derefa. Waziri Jafo aliagiza mwananchi huyo alipwe fedha zake zote zilizobaki ifikapo saa 10 jioni jana.

Viongozi hao waliwekwa ndani jana saa nne asubuhi wilayani Mwanza baada ya mkazi wa kitongoji chaIbisabageni Christopher Derefa kumlalamikia Magesa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo kwamba amekataa kumlipa fidia iliyobaki ya shamba lake kwenye eneo la Bukara wilayani Sengerema.

“Ninyi mmedanganya vyombo vyote vya Serikali, wakati mkijua nyie ni watumishi wa umma, katika swala la maadili mmefanya kosa kubwa sana la kimaadili na mmenipa ishara kwamba nyie hamuendisite( eneo) kushughulikia matatizo ya wananchi, wewe Mkurugenzi unashindwa kufika shambani”amesema Mongela.

Awali, Derefa alimweleza Waziri Jafo kuwa alikuwa alipwe fidia ya Sh 4,686,464/- lakini badala yake amepwa kiasi cha Sh 1,496,874/- hivyo bado anaidai halmashauri hiyo Sh 3,189,590/-

Wanafunzi kusoma kwa zamu- Dar
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 6, 2021