Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Tabora, Aggrey Mwanri amechukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Siha, Mkoani Kilimanjaro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Serikali ilitangaza kustaafu kwake Ukuu wa Mkoa wa Tabora Julai 03, 2020, leo amekabidhiwa fomu na Katibu wa CCM Wilaya ya Siha, Mwanaidi Mbisha katika Ofisi za CCM Wilaya.

Hadi Bunge linavunjwa Juni 16 mwaka huu, Jimbo hilo lilikuwa chini ya Naibu Waziri wa Afya wa sasa, Dkt. Godwin Mollel aliyejiunga CCM mwaka 2017 akitokea CHADEMA.

Aggrey Mwanri akikabidhiwa fomu

Mwanasheria mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Philip Filikunjombe akitoka ofisi za CCM wilaya ya Ludewa mkoani Njombe mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya ubunge jimbo la Ludewa kupitia CCM.

Dkt. Philip Filikunjombe akisaini kuchukua fomu


Aliyekuwa Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro amejitokeza katika ofisi za CCM Wilaya ya Arusha kuchukua fomu za kuwania kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Arusha Mjini.

Kalist Lazaro akikabidhiwa fomu

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo, amechukua fomu ya kuomba ridhaa Chama cha mapinduzi kimteue agombee ubunge Jimbo la Kisarawe. Waziri Jafo ameijaza fomu hizo hapohapo na kisha kuzirudisha.

Selemani Jafo, akikabidhiwa fomu

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye amechukua fomu ya kuomba kupitishwa kugombea ubunge Mbozi Mkoa wa Songwe kupitia CCM, Simbeye amekabidhiwa fomu na katibu wa CCM Wilaya ya Mbozi Julius Mbwiga.

Godfrey Simbeye akikabidhiwa fomu.

36 wachukua fomu kuwania ubunge jimbo la Bukoba mjini
Picha: Wagombea CCM waliochukua fomu, Mtoto wa Lowassa akiwemo

Comments

comments