Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema bado nia yake ya kukutana na Watengenezaji wa pombe aina ya gongo ipo palepale.

Amesema, lengo ni kujadiliana na kuona namna nzuri ya kuiboresha pombe hiyo kwa kuipelekea TBS na kwa Mkemia ili ipimwe na kuondoa sumu.

Amesema, badala ya kuikuza na kuona kuwa hapa kuna kitu kinaweza kutupeleka kwenye viwanda, tunazuia. Je, mnaokunywa hizo pombe za viwandani mnajua asili yake?.

Amehoji, “Kwanini gongo haitambuliwi kama kinywaji halisi cha Kitanzania?” Na kusisitiza kuwa atakutana na Watengenezaji wa gongo ili waone namna ya kuiboresha.

Ikumbukwe kuwa Katika Mkutano wa 11, Kikao cha 4 cha Bunge la Aprili 11, 2008, aliyekuwa Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge alisema lililozingatiwa katika kupiga marufuku pombe aina ya gongo ni njia inayotumika kutengenezea si inayozingatia usafi na afya ya binadamu.

TRC yarejesha safari za Treni Kilosa
Bashiru: Katiba mpya ni ajenda ya kudumu