Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu,  Zelote Stephen ameionya idara ya uvuvi iliyo chini ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini kuhakikisha wanawachukulia hatua wale wote wanaokamatwa na zana haramu za uvuvi na kutangaza hukumu zao na si kuishia kwenye kuchoma zana zao tu.

Ameyasema hayo wakati akiteketeza zana haramu zilizokamatwa kupitia doria katika vijiji vya Kabwe, Isaba, Chongokatete, mandakerenge, kolwe, lupata na kisenga katika Wilaya ya Nkasi Mkoani humo, ambapo zoezi hilo lilifanyika katika mwalo wa kijiji cha Kirando.

“Kukamata na kuchoma haitoshi, kwasababu hii inaungua tu, nataka tuwachome wahalifu kwa kutumia sheria, nimechoma sana nyavu hizi na huu mtindo bado unaendelea, hii haina tija, kila tukichoma madhara yanatokea, mazingira yanaharibika, sasa tuseme basi, ningependa kusikia mhalifu kakamatwa kapelekwa mahakamani na kupewa adhabu,” Amesema

Aidha,  Zelote amewaasa watumishi wa Idara hiyo kuachana na kupokea rushwa, jambo ambalo linaonekana kukwamisha juhudi za serikali katika kulinda rasilimali zake kwaajili ya faida ya kizazi hiki na kijacho.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa wananchi bado wanahitaji kuendelea kupatiwa elimu juu ya umuhimu wa rasilimali hizo na wajulishwe kuwa rasilimali hizo ni za watanzania wote na hatimae kuacha tabia kuvua samaki hao kwa zana zisizokubalika na sheria za serikali.

 

Kamati ya bunge yakwama kutoa ripoti ya Lissu
Kendrick, Dj Khaled watajwa zaidi tuzo za BET