Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martine Shigela amepiga marufuku Askari wa jeshi la akiba (mgambo), kufanya operesheni yoyote ya kuwaondoa wafanyabiashara ndani ya Mkoa huo.

Kauli hiyo ya Shigela imekuja baada ya Rais Samia kuwafuta kazi Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa na Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Sheila Lukuba baada ya kushindwa kushughulikia namna ya kuwapanga machinga na kusababisha ugomvi kati yamakundi hayo na kusababisha hasara kwa wafanyabiashara.

Shigella amesema, “nitoe maelekezo kuhusiana na jeshi letu la mgambo walioajiriwa kwenye halmashauri ya manispaa ya Morogoro, kuanzia leo sitaki tena kuwaona wakifanya oparesheni zozote ndani ya Mkoa wetu wa Morogoro.”

Ajibu aachwa Dar es salaam
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 17, 2021