Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amewatahadharisha wakurugenzi wa halmashauri pamoja na madiwani juu ya kuanzisha vyanzo vipya vya mapato ili kuweza kufikia malengo zaidi ya waliyowekewa na Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
 
Wizara ya OR – TAMISEMI imesema kuwa itawapima wakurugenzi kulingana na makusanyo ya mapato yao na kuwataka hadi kufikia mwishoni mwa mwaka wa fedha 2018/2019, halmashauri zimetakiwa kufikia asilimia 81 ya ukusanyaji wa mapato.
 
Aidha, katika kuhakikisha azma hiyo inafikiwa, Wanagbo amewaomba madiwani kuhakikisha kila vikao vyao vinapofanyika agenda ya mapato ipewe kipaumbele.
 
“Waswahili wanasema ‘mchelea mwana kulia hulia yeye’ sasa kama tutawalealea hawa ambao wanatusababishia sisi tusikusanye mapato matokeo yake mkichelea kwenu nyinyi kama viongozi na wawakilishi wa wananchi mtakuja kuhukumiwa kule kwenye kura,“amesema Wangabo.
 
  • Mambosasa: Tukio hili limefanywa na wazungu wawili
 
  • Makonda akanusha taarifa za kupatikana kwa Mo’ Dewji
 
  • Tamko la Kangi Lugola sakata la kutekwa kwa Mo Dewji
 
Hata hivyo, Wangabo amezipongeza Halmashauri ambazo zimevuka lengo la makusanyo lililowekwa na Wizara kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ambapo Halmashuri mbili za Wilaya ya Nkasi pamoja na Wilaya ya Sumbawanga zilikusanya kwa asilimia 90, huku Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ikiwa imekusanya kwa asilimia 63 na Manispaa ya Sumbawanga ikiwa imekusanya kwa asilimia 53

Dereva wa Mo Dewji afunguka, ‘alipokea meseji za vitisho’
Majaliwa amtaka DC Shekimweri kufanya uchunguzi