Uongozi wa klabu ya Espanyol umeendelea kuwawekea ngumu Real Madrid katika harakati zao za kutaka kumsajili mlinda mlango Kiko Casilla ambaye anatazamwa kama mrithi wa Iker Casillas aliyetimkia FC Porto.

Raisi wa klabu ya Espanyol, Joan Collet amewasisitiza viongozi wa klabu hiyo ya mjini Madrid kuongeza ofa yao kutoka paund million mbili endapo wanahitaji kumsajili mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 28.

Collet amesema hatokua tayari kukaa meza moja na viongozi wa klabu ya Real Madrid kujadili suala la uhamisho wa Casilla, kama hataona ofa zaidi ya paund milioni 4 ambazo ni sawa na Euro milioni 2.8.

Real Madrid wameonyesha kujiegemeza Espanyol, baada ya kupata changamoto kubwa katika jaribio lao la kutaka kumsajiuli mlinda mlango wa Man Utd David De Gea.

Man Utd Kumruhusu Chicharito Wakiridhishwa
Azam FC Watimiza Ndoto Za Kumsajili Mshambuliaji Wa Kinyarwanda