Rais wa klabu ya Real Madrid,  Florentino Perez anatarajia kutuma ofa ya mwisho nchini Uingereza kwa ajili ya kuushawishi uongozi wa klabu ya Man Utd kuridhia kumuachia mlinda mlango, David de Gea .

Gazeti la The Sun la nchini Uingereza limeripoti kuwa kiongozi huyo amepanga kutuma ofa ya Pauni milioni 50 ambayo anaamini itatosha kumsajili De Gea ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani sambamba na wachezaji wenzake wa Man utd wakijiandaa na msimu mpya wa 2017/18.

Perez amedhamiria kuona uhamisho wa mlinda mlango huyo kutoka nchini Hispania ukikamilishwa katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi, kutokana na hitaji lililopo kwenye kikosi cha Real Madrid.

Hii si mara ya kwanza kwa Real Madrid kuonesha nia ya kutaka kumsajili De Gea, kwani waliwahi kufanya hivyo mwaka 2015, lakini taratibu za uhamisho zilikwama dakika chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

De Gea mwenye umri wa miaka 26, kwa sasa ana mkataba wa miaka mitano ambao unamuwezesha kuituikia Man Utd hadi mwaka 2022, lakini bado anaonesha kuwa tayari kurejea nyumbani kwao Hispania.

Mwakyembe: Serikali hairidhishwi na kampuni ya ubia kati ya TBC na Star Times
Meya wa jiji la Dar awafunda wajasiliamali