Vinara wa ligi kuu ya soka nchini Hispania (La Liga) Real Madrid wanataka kucheza mchezo wa pata potea kuhusu hali ya mshambuliaji wao wa pembeni Gareth Bale ambaye yupo shakani kuukosa mchezo wa mwishoni mwa juma lijlo dhidi ya FC Barcelona.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Wales aliumia kifundo cha mguu katika mchezo wa mzunguuko wa tano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Sporting Lisbon, uliochezwa jumanne mjini Lisbon.

Taarifa zilizochapishwa katika tovuti ya klabu ya Real Madrid zimeeleza kuwa, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 huenda akapata ahuweni na kuwahi mazoezi ya kikosi cha Real Madrid kuelekea katika mpambano wa El Classico.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa “Bale atakua chini ya uangalizi wa kitatibibu na huenda kaanza mazoezi mepesi, kulingana na matarajio ya kupata ahuweni ya jerahe lake la kufundo cha mguu, ”

“Kuna uwezekano mkubwa wa kuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri kuelekea mjini Barcelona Disemba 03.” Ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeleta mashaka miongoni mwa mashabiki ambao wanahisi huenda kuna ajenda ya makusudi ya kumuharakisha Bale ili acheze mchezo dhidi ya FC Barcelona, jambo ambalo wanahisi litawagharimu kwa kiasi kikubwa na kuhatarisha afya ya mshambuliaji huyo.

Man Utd Kumbembeleza Zlatan Ibrahimovic
Video: Makonda awataka watumishi kubandika majukumu yao kwenye mbao za matangazo ya ofisi