Klabu ya Real Madrid, huenda ikafanya dili la kubadilishana wachezaji na Chelsea, kufuatia mpango wa kutaka kuboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Real Madrid, wanatajwa kufanya mipango ya kukamilisha dili hilo, kwa kumtazama kwa jicho la tatu kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji, Eden Hazard ambaye yupo kwenye rada za klabu kadhaa za barani Ulaya.

Mshambuliaji kutoka nchini Colombia, James Rodriguez ametajwa kuingia katika mpango wa kubadilisha na Hazard ili aweze kuelekea nchini Hispania kucheza soka na klabu Real Madrid, yenye historia kubwa barani Ulaya.

Sababu kubwa ya Rodrigues, kuingia katika mpango wa kubadilishana, umekuja kufuatia kiwango chake dhaifu ambacho kimeonekana katika msimu huu wa ligi, ambapo tayari imedhihirika Real Madrid hawatoweza kutwaa ubingwa wa nchini Hispania.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, alitarajiwa kuonyesha uwezo mkubwa tangu aliposajiliwa huko mjini Madrid, mwaka 2014, baada ya kusajiliwa kwa ada ya uhamisho wa paund million 70, akitokea AS Monaco, lakini imekua tofauti.

Hazard, mwenye umri wa miaka 25, amekua hana mzimu mzuri katika klabu ya Chelsea, kutokana na tetesi kueleza kwamba alikua na mikwaruzano na meneja aliyetimuliwa kazi Jose Mourinho, hali ambayo ilisababisha kiwango chake kuporomoka.

Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane anaamini endapo atafanikisha, usajili wa Hazard, kutakua na uhai katika kikosi chake huku akiamini kiwango cha mchezaji huyo kitarejea maradufu.

Wakati Real Madrid, wakifikiria mpango huo, Chelsea walishawahi kutangaza thamani ya Hazard, ambayo ilifikia paund million 100, huku ada yake ya uhamisho iliyomtoa nchini Ufaransa akiwa na klabu ya Lille ikiwa ni paund million 34.

Ratiba Ya Nusu Fainali Ya Emirates FA Cup Yapangwa
Kinnah Phiri Ataja Sababu Za Kufungwa Na African Sports