Mabingwa wa soka barani Ulaya, Real Madrid watatumia mbinu mbadala za kutaka kushinda mtihani wa kumsajili kiungo kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Juvetuns ya Italia, Paul Pogba, ambaye ni gumzo kwa sasa katika harakati za usajili.

Real Madrid wanatarajia kutumia mbinu za kumtanguliwa kiungo wao kutoka nchini Ujerumani Toni Kroos sambamba na kikasi cha pesa ili kufanikisha mpango wa usajili wa Pogba.

Gazeti la Le 10 Sport la nchini Hispania, limeripoti kwamba, Real wamedhamiria kufannya hivyo kufuatia upinzani mkali wanaoupata kutoka kwa Man Utd ambao wapo katika harakati za kumsajili Pogba kutoka Juventus.

Juve wamepanga kumuuza kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, kwa kiasi cha Euro milion 120.

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez anaamini thamani hiyo huenda ikawa sahihi kwa Paul Pogba, lakini anaona ni rahisi kwake kumruhusu Kroos kuondoka na kumfanywa sehemu ya dili hilo.

Mbali na Krros, pia mshambuliaji kutoka nchini Colombia James Rodriguez, naye anatajwa huenda akaingizwa katika mpango wa kubadilishana.

Pablo Zabaleta Asaka Njia Ya Kumuepuka Guardiola
Vincenzo Montella Akabidhiwa Mikoba Ya AC Milan