Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya inaendelea leo usiku huku mchezo unaowakutanisha vijana wa Mauricio Pochettino, Tottenham na mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa Real Madrid ukitarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi wa soka duniani.

Tottenham wanawakaribisha Real Madrid katika uwanja wa Wembey huku mchezo uliopita uliopigwa katika dimba la Santiago Bernabeu  ukimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.

Kurejea kwa mshambuliaji Gareth Bale ambaye aliukosa mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo kutokana na majeraha itakuwa ni chachu ya kuongeza mvuto na nguvu katika kikosi cha Zidane ikizingatiwa kuwa Bale anarudi kucheza dhidi ya klabu yake ya zamani.

Kikosi cha Zinedine Zidane kinaigia dimbani leo kikiwa na kumbukumbu ya kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa klabu ya Ginora kwenye mchezo uliopita wa ligi kuu ya Hispania La Liga.

Tottenham nao watakuwa na mshambuliaji wao tegemeo Harry Kane ambaye alikosa katika mchezo wa ligi kuu ya Epl, mchezo ambao Tottenham ilifungwa na Man Utd bao 1-0.

Madrid na Tottenham wote wanalingana pointi katika kundi H wakiwa na pointi 7, wamefunga mabao 7 na wote wameeruhusu mabao 2 baada ya kucheza michezo mitatu.

 

Nyalandu: kilichobaki kwa sasa ni kuimarisha Demokrasia
Vifaranga vyenye thamani ya shil. milioni 12.5 vyateketezwa kwa moto