Klabu Real Madrid ya Hispania imetwaa taji la ubingwa wa La Liga baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Malaga na kumaliza ukame wa miaka mitano bila kutwaa kombe hilo.

Aidha, katika mchezo huo Real Madrid ilikua inahitaji pointi moja kabla ya mchezo huo walianza kupata bao la kuongoza katika dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa Cristiano Ronaldo, kisha Karim Benzema akifunga bao la pili katika dakika ya 55.

Real Madrid wamemaliza msimu wakiwa na pointi 93 kwa michezo 38 wakifuatiwa na mahasimu wao Barcelona waliomaliza na pointi 90 baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Eibar.

Hata hivyo, katika ligi hiyo Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi ameibuka kidedea kwa kuwa mfungaji bora wa ligi hiyo akimaliza na mabao 37, akifuatiwa na Luis Suarez, mwenye mabao 29, Cristiano Ronaldo akiwa katika nafasi ya tatu kwa magoli 25.

Bibi vizee vya Turin vyaweka historia Ligi Kuu ya Italy
Serengeti Boys yang'olewa katika michuano ya AFCON U-17