Kiungo Mshambuliaji Ramadhan Chombo ‘Redondo’ ameweka wazi ataachana na Biashara United Mara mwishoni mwa msimu huu, baada ya kumaliza mkataba wake.

Redondo ametoa kauli hiyo, huku Biashara United Mara ikibakisha michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22, ikiwa katika hali mbaya ya kuchungulia shimo la kushuka daraja.

Amesema tayari ameshapata klabu ya kuitumikia msimu ujao, lakini anasubiri siku na saa maalum, ili kuweka wazi kwa ajili ya mashabiki wake ambao wana hamu ya kujua wapi atakapocheza msimu ujao.

“Msimu ujao nitakuwa timu nyingine, tuombe uzima tu. siwezi kutaja timu kwa sasa kwani bado nipo Biashara United Mara na ligi hajiamalizika, ila siku si nyingi nitasema,” amesema Redondo.

Ramadhan Chombo ‘Redondo’ alisajiliwa Biashara United Mara misimu mitatu iliyopita, na kwa kipindi chote ameonyesha kuwa na kiwango bora, ambacho kilikua msaada mkubwa kwa timu hiyo ya mjini Musoma-Mara.

Kifo cha Maradona wauguzi Kortini
Mauzo medali ya dhahabu kusaidia watoto wakimbizi