Mwamuzi maarufu wa mchezo wa mpira wa miguu nchini Somalia amepigwa risasi na kuuawa karibu na nyumbani kwake mjini Mogadishu.

Osman Jama Dirah, ambaye alijichukulia umaarufu mkubwa katika nafasi ya Mwamuzi mara baada ya kuchezesha michezo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Refa huyo alikuwa anapendeka na wanamichezo wengi nchini humo alipigwa risasi akitokea msikitini karibia na nyumbani kwake mtaa wa Wardhigley.

Aidha, taarifa zimesema kuwa watu wawili waliokuwa wamepakizana kwenye pikipki walimfyatulia risasi kisha kutokomea kusikojulikana, hivyo kusababisha pigo kubwa katika chama cha mpira nchini humo na Afrika kwa ujumla.

Hata hivyo, Mwamuzi huyo alianza kazi hiyo mwaka mwaka 1997, mara baada kukizi vigezo vya Shirikisho la Mpira wa Miguu ulimwenguni FIFA hivyo kuanza kazi hiyo rasmi.

Video: Nchemba aahidi mifuko 200 ya saruji shule ya msingi Ujungu
Prof. Maghembe awataka wanaoishi pori tengefu wahame