Maria Paraskeva, mwanamke kutoka  nchini Cyprus, ndiye mwanamke aliyeweka rekodi ya kuvaa vazi la harusi refu zaidi Duniani.

Maria aliolewa mnamo Agosti 2018, lengo lake kubwa halikuwa tu kusema , “Nimekubali kuolewa.” Hapana, alidhamiria pia kuweka rekodi kupitia tukio la ndoa yake.

“Ndoto yangu tangu nikiwa mtoto siku zote ilikuwa ni kuvunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kuvaa gauni refu zaidi” alieleza.

Maria Alitimiza ndoto yake kwa kuvaa gauni lenye mkia wenye takribani futi 22,843 na inchi 2.11, Sawa na urefu wa viwanja vya mpira wa miguu 63.5.

Mbunifu maarufu wa mavazi Virginia Abloh afariki Dunia
Zion Clark-mpigana mieleka asiye na miguu na maajabu yake.