Mshambuliaji wa Namungo FC ya Lindi Reliants Lusajo amesema kuna vitu vingi anawashauri viongozi wa klabu hiyo kwenye upande wa masoko na kufanikiwa kupata wadhamini kadhaa msimu huu.

Lusajo ambaye ana Degree ya Procurement and Supply Management anasema kuna wakati klabu hiyo ilitaka kumpa kazi kutokana na elimu yake ili aisaidie klabu maeneo tofauti.

“Namungo bado timu changa lakini wana mikakati yao na tunashauriana kwa sababu mimi naweza pia kufanya mambo ya marketing kwa hiyo nimeshawashauri vitu vingi.”

“Kuna wakati walitaka kuniajiri katika eneo hilo, timu inatakiwa kuangalia fursa mbalimbali ikiwemo kuuza jezi na vitu vingine vingi. Kama nitaendelea kubaki Namungo, tutaendelea kufanya vitu vikubwa zaidi.”

“Siwezi kusema nimesaidia Namungo kupata wadhamini kwa asilimia zote lakini kuna vitu huwa nashauri viongozi lakini huwa kuna uzito fulani hivi kwa sababu viongozi wetu bado wageni kidogo kwenye mpira lakini kama tutakuwa pamoja huko mbele watafanya vitu vikubwa.”

Kuhusu tetesi za usajili zinazomuandama katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu wa 2019/20, Lusajo amesema endapo atasajiliwa na Young Africans, anaamini hakuna kitu kitamfanya ashindwe kuyafanya yale yote anayoyafanya sasa kunako klabu ya Namungo.

Lusajo anashika nafasi ya pili kwenye orodha ya vinara wa mabao ligi kuu ya Vodacom akifunga mabao 11 sawa na Yusuf Mhilu wa Kagera Sugar.

“Ninaamini kwamba uwezo wa mchezaji huwa haujifichi, iwapo nitapata nafasi ya kusajiliwa Yanga, nitaendelea na kasi yangu ya kutupia pale nitakapopata nafasi “Uzuri ni kwamba kwa sasa nimezidi kuimarika na kuwa na uwezo wa kufunga jambo ambalo linanifanya niamini kwamba ninaweza kucheza popote ndani na nje ya Tanzania,” amesema

Nyota huyo msomi aliwahi kuwatumikia young Africans mwaka 2013 ikielezwa kocha Luc Eymael amempendekeza miongoni mwa wachezaji wazawa aliopanga kuwasajili.

WHO wamjibu Trump, "hatuna upendeleo"
Sven Vandenbroeck: Timu zipewe muda wa kujiandaa