Meneja wa klabu ya Aston Villa, Remi Garde huenda akaondoka juma hili na kuachia majukumu yake kwa meneja mwingine kutokana na hali kumuendea kombo tangu alipokabidhiwa kikosi mwezi Novemba mwaka 2015.

Kwa mujibu wa gazeti la The Telegraph, meneja huyo amebakiwa na muda wa saa 48, kabla ya kutii amri itakayotolewa na viongozi wa ngazi za juu wa Aston Villa ambao wamechoshwa na huduma yake.

Mwenyekiti wa Aston Villa, Steve Hollis amekua katika vikao muhimu na viongozi wengine wa klabu hiyo, na agenda kubwa inayojadiliwa humo ni mustakabali wa meneja huyo kutoka nchini Ufaransa, ambaye ameshindwa kuipatia matokeo mazuti The Villians.

Aston Villa, bado inaburuza mkia wa msimamo wa ligi ya nchini England, huku michezo minane ikiwa imesalia kabla ya msimu huu kufikia kikomo, hali ambayo huenda ikaisababishia klabu hiyo kushuka daraja na kushiriki ligi daraja la kwanza msimu wa 2016-17.

The Telegraph believe Nigel Pearson is Villa's preferred candidate to take overNigel Pearson alipokua meneja wa Leicester City alifuatilia moja ya michezo ya ligi kuu ya soka nchini England

Wakati gazeti la The Telegraph, likiripoti taarifa za kuondoka kwa Remi Garde, gazeti la The Daily Mail lenyewe limeibuka na taarifa zinazomtaja aliyekua meneja wa klabu ya Leicester City, Nigel Pearson kuchukua nafasi yake huko Villa Park.

Pearson, huenda akakabidhiwa jukumu hilo, kwa kuwa na sifa ya kuweza kupambana katika ligi daraja la kwanza endapo itatokea Aston Villa inaporomoka daraja, huku kumbukumbu zikionyesha kwamba alifanya vyema wakati akiisaidia Leicester City, kucheza ligi kuu mwaka 2014.

Garde tangu alipokabidhiwa kikosi cha Aston Villa, amepoteza michezo 12 miongoni mwa michezo 20 aliyoishuhudia kama mkuu wa benchi la ufundi, hali ambayo imechangia kufikisha The Villians ilipo sasa.

Jahazi La Man City Linavyoendelea Kuzamishwa Na Majeruhi
Djokovic Achuana Na Rafael Nadal Kuweka Rekodi Ya Masters Crown