Rapa wa kike, Remy Ma amechochea kuni kwenye moto wa bifu yake na Nicki Minaj baada ya kumjekeli kwenye Tuzo za Video za Muziki za MTV (MTV VMA 2017).

Remy ambaye alikuwa mshereheshaji msaidizi wa tukio hilo (cohost) akimsaidia Terrence J, alimtaja Nicki Minaj kwa kejeli akiyarudia maneno ambayo hasimu wake huyo aliyatumia mwaka 2015 kwenye tuzo hizo kumkejeli Miley Cyrus.

Wakati tamasha hilo lilipokuwa katika mapumziko kwa ajili ya matangazo ya biashara, Terrence J na Remy Ma walitumia sekunde 30 kuwaeleza watazamaji kinachofuata ambapo Remy alisikika akifunguka mwishoni, “Nicki-What’s good?” (niaje..!)

Maneno hayo aliwahi kuyatumia Nicki Minaj kwenye tuzo za MTV VMAs mwaka 2015 akimkejeli Miley Cyrus ambaye alikuwa amemkosoa vikali kwenye mahojiano yake na jarida la New York Times lililotoka wiki chache kabla ya kufanyika kwa tuzo hizo. Nicki alishinda tuzo na kurusha kejeli yake.

Ikumbukwe kuwa Nicki Minaj na Remy Ma waliingia kwenye bifu la wazi miezi kadhaa iliyopita hususan baada ya Remy kuachia wimbo wenye makombora mazito kwa Nicki Minaj kupitia ‘Shether’. Ngoma hiyo iliachiwa Februari mwaka huu.

Mkuu wa Wilaya atoa agizo zito makanisani
Masau Bwire Aibuka Tena, Asema Bao La Ngoma Halina Utata