Siku moja baada ya mashabiki wa Diamond kuhamaki kutokana na uamuzi wa rapa Rick Ross kufuta picha karibu zote za Diamond kwenye mtandao wake wa Instagram, rapa huyo amewashusha pumzi.

Kutokana na maswali mengi yaliyokuwa yanamiminika kwenye ukurasa wa instagram wa wa Bosi huyo wa MMG kutaka kujua kama ameanzisha uhasama na Diamond, ameamua kujibu kiutuuzima kupitia picha moja aliyoipost Disemba Mosi mwaka jana, ambayo ndiyo pekee ilikuwa imesalia.

Rick Ross ameweka ‘comment’ katika orodha ya zile za mashabiki na kuandika ‘Diamond is a Legend’. Kwa tafsiri isiyo rasmi, ‘Diamond ni nguli’.

Wachambuzi wa masuala ya burudani wanaeleza kuwa huenda Rick Ross alifuta picha zote ambazo zina uhusiano na kinywaji cha Belaire kwa sababu za kibiashara.

Video ya wimbo wa Diamond aliomshirikisha Rick Ross pamoja na matangazo ya wimbo huo karibu yote yalikuwa na uhusiano na kinywaji hicho.

Aliyemmwagia mwanaye tindikali aachiwa, Mahakama yaridhia sababu
Kizimbani kwa kumbaka mfanyakazi wake ofisini