Rapa Rick Ross amekuwa msanii wa kwanza kusimama na Cardi B kwenye wikii hii ngumu ya mashambulio ya watu Tweeter na mitandao mingine ya kijamii baada ya Cardi B kutoa kauli kuwa aliwahi kutumia madawa ya kulevya kuwalewesha wanaume na kuwaibia kipindi anafanya kazi ya uchojoaji (stripper).

Kupitia akauti yake ya snapchat rapa huyo amemtetea Cardi B kwa kusema hayo ni mambo ya zamani na yamepita hayaathiri chochote kwenye maisha yake kwasababu ile ilikuwa ni “lifestyle” yake ya kipindi hicho

Rick Ross amesema, hata yeye amewahi kufanya makosa kwa kutoa mfano kuwa aliwahi kuiba gari zamani lakini haikumzuia yeye kuendelea kufanya kazi na mashabiki.

Hata hivyo mashabiki wamekuwa wakiendelea kumtupia lawama rapa Cardi B aliyetoa kauli hiyo kupitia insta stori yake kwa baadhi ya watu kudai kuwa Cardi anatakiwa kuchukuliwa hatua kali kwa alichikifanya.

Aidha lawama zimeendelea kutolewa kwa mashirika ya haki za binadamu kuwa yanaangalia upande mmoja tu wa haki za wanawake katika kesi za unyanyasaji wa kijinsia na kusahau upande wa wanaume.

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Machi 30, 2019
Elimu bora ndio msingi wa maendeleo- Majaliwa

Comments

comments