Kwa mara ya kwanza Rapa wa Marekani, Rick Ross, amewasili  jijini Nairobi, nchini Kenya kwa ajili ya kufanya shoo ambayo inafanyika leo (Jumamosi) katika viwanja vya Carnivore.

Msanii huyo ambaye ni maarufu kwa kufanya shoo akiwa kifua wazi, alionekana kupungua kidogo umbo lake ambalo mashabiki wake wamelizoea.

Kwa mujibu wa kituo cha Radio NGR ambao ndio walioandaa tamasha hilo wamesema, Ross ambaye ni maarufu kwa jina la Boss, atatumbuiza na wasanii maarufu wa Kenya, Khaligraph Jones, Camp Mullah na Nyashinski.

Kwa Afrika Mashariki rapa Rick Ross amezidi kupata umaarufu wake mara baada ya kufanya ngoma na msanii wa Tanzania anayefanya vizuri kitaifa na kimataifa Diamond Platinumz na wimbo wake wa Waka waka, ambao uliingia katika mgogoro na BASATA pamoja na TCRA kutokana na maudhui ya nyimbo hiyo.

Aidha msanii Rick Ross amewahi kutua nchini Tanzania mwaka 2012 kutumbuiza katika tamasha la Fiesta ambao hufanyika kila mwaka na wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania..

 

Basi lapata ajali mkoani Kagera
Kansela wa Ujerumani akutana na Trump

Comments

comments