Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete amesema kuwa ingawa yeye ni mtu wa dini, familia yao huwa haiachi kukumbuka utamaduni wa ibada ya kale ya kimila.

Akizungumza jana katika mahojiano na Sun Rise ya 100.5 Times Fm, Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete alisema kuwa wazazi wake wamekuwa wakiwakumbusha walikotoka hivyo huenda kuomba na kushukuru mizimu ya kwao.

“Uzuri wa mzee wangu mimi, siku zote ametulea kwa kutukumbusha tulikotoka. Kwa wazee waliotutangulia, kwa mfano katika kipindi ambacho hakuna mvua, walikuwa wanaomba na mambo yanaendelea kawaida. Ulikuwepo ni utamaduni wetu,” alisema.

“Sasa mara kwa mara kunapokuwa na haja ya kufanya hivyo, au hata wakati ambapo hakuna haja ya kufanya hivyo huwa tunaenda kushukuru, sio lazima uwe na shida ili uende,” aliongeza.

Alisema kuwa hufanya hivyo mara kwa mara na angalau kila mwisho wa mwaka kwa lengo la kushukuru.

Gareth Southgate Awakuna Viongozi Wa FA
Abracadabra Awaburuza Tena Sweden