Katika kuongezea nguvu juhudi za kuboresha elimu nchini, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ametoa msaada wa vitabu vya sayansi na hisabati jimboni kwake vyenye thamani ya shilinigi milioni 70.

Mbunge huyo akishirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la Kulea Childcare, walitoa jumla ya vitabu 3,438 hivi karibuni kwa shule za msingi na sekondari jimboni humo.

Ridhiwani alieleza kuwa vitabu hivyo vitagawiwa kwa tarafa tano zinazopatikana kwenye Halmashauri ya Mji wa Chalinze ambapo kila tarafa itapata vitabu 610 ikiwa ni pamoja na tarafa ya Chalinze iliyopewa vitabu 998.

Walimu wa Halmashauri hiyo waliupokea msaada huo kwa moyo wa shukurani, lakini walimtaka Mbunge huyo kufikisha kilio chao Serikalini kuhusu upungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

“Tuna upungufu mkubwa wa walimu wa Sayansi na Hisabati. Kila shule ina upungufu wa walimu wasiopungua watano. Tunaomba serikali ituongee walimu,” alisema Mwalimu Komba ambaye alizungumza kuwawakilisha walimu wenzake.

 

Unyama: Awachinja watu 14 wa familia yake wakiwemo wazazi na wanae
Kapombe wa Azam ashinda tuzo hii nzito ya Ligi Kuu