Kumekuwa na tetesi zinazosambaa kuhusu Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete zikidai anampango wa kugombea uongozi katika klabu ya Yanga, ambapo Ridhiwani amekanusha tetesi hizo na kudai kuwa hana mpango wa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mwenyekiti na kujiuzulu nafasi hiyo, Yusuph Manji.

”Sina lengo lolote la kutaka uongozi ndani ya Yanga labda wanachama wenyewe ndio wanatengeneza maneno hayo lakini mimi binafsi hakuna sehemu nimewahi kutamka;” amesema Ridhiwani.

Ridhiwani ambaye ni shabiki wa klabu hiyo amesema yeye sio mwanachama wa timu hiyo hivyo sio rahisi kugombea kiti hiko kwani hata kadi ya uanachama hana.

Yusuph Manji alichukua uamuzi wa kujiuzulu kiti cha uenyekiti wa klabu hiyo kutokana na shutuma mbalimbali zilizokuwa zinamkabili ambazo zilichangiwa na baadhi ya viongozi wa serikali, na wengine kutoka ndani ya yanga ambao wanatumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kwa maslahi yao binafsi na sio ya yanga.

Mpaka sasa Timu ya Yanga haijapata mwenyekiti wa kushikilia nafasi ya Manji hata hivyo baadhi ya mashabiki wanadhani kufanya vibaya kwa timu hiyo msimu huu ni kutokana na timu hiyo kukosa kiongozi mfadhili kama ambavyo alikuwa Manji.

Umoja wa Ulaya wapingana na Trump kuhusu Iran
Ndugu wadai rambirambi za Masogange bongo movie waamua yao